Update:

Ajali yaua watatu mkoani Njombe

Watu Watatu  wamekufa na wengine 28 kujeruhiwa  katika ajali ya gari iliyohusisha basi  la Ilyana mkoani Njombe .

Basi hilo lenye namba T 202 Dgk lilikuwa likifanya safari zake kutoka jijini dsm ,kwenda mkoani Ruvuma, ambapo waliofariki katika ajali hiyo ni wanaume Wawili na mwanamke Mmoja.

Kamanda wa polisi  mkoa wa Njombe Pudensiana Protas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo  katika  eneo la Image kata ya Igominyi baada ya basi hilo kupinduka majira ya saa mbili  usiku wa jana.

Kamanda Protas amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi  wa gari hilo ambapo ametoa wito kwa abiria kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama mara dereva anapoendesha gari kwa mwendokasi ili kuepusha ajali.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Njombe  huku majeruhi wa ajali hiyo wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

No comments