Update:

03 February 2017

Waziri Mkuu asema Rais hajawahi kutangaza kuviua vyama vya siasaWaziri mkuu KASSIM MAJALIWA amesema Rais DKT JOHN MAGUFULI hajawahi kutangaza kuviua vyama vya upinzani ifikapo mwaka 2020.

Waziri mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya papo kwa papo ambapo alijibu swali la Mbunge wa Hai FREEMAN MBOWE kuhusu kufungwa jela kwa baadhi ya wafuasi wa chama cha Demokrasia na maendeleo – CHADEMA.

Kuhusu suala la uhaba wa chakula waziri mkuu amesema tayari ufafanuzi umetolewa na serikali na kuhamasisha wafanyabiashra kufanya biashara ya chakula kati ya maeneo yenye chakula na yale ambayo hayana.

Katika hatua nyingine bunge limeahirisha kusomwa kwa mara ya pili kwa muswada wa sheria ya madaktari wa meno na wataalamu wa afya shirikishi wa mwaka 2016 .

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto UMMMY MWALIMU amesema kinachofanyika ni kutaka kuwatambua na kuwasajili kutokana na elimu zao.