Update:

16 February 2017

Wazee wa kimila wahusishwe migogoro ya ArdhiWAZIRI mkuu KASSIM MAJALIWA amesema Viongozi wa dini pamoja na Wazee wa kimila ni Watu muhimu kushirikishwa katika kutatua migogoro ya Ardhi ili kuondoa chuki na mipigano yasiyo ya lazima katika Jamii.Akizungumza na Watumishi wa umma, viongozi wa dini pamoja na baadhi ya Wazee wa mila wilayani KITETO mkoani MANYARA, Waziri mkuu amesema imani na busara za viongozi hao zinamchango mkubwa katika kuleta amani nchini.Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa MANYARA Dakta JOEL BENDERA amesema wilaya ya KITETO iliyokuwa na mapigano kwa sasa hali imekua tulivu na amani.