Update:

16 February 2017

Tume yaundwa kuchunguza moto ulioteketeza mabweni ya shule ya ITAMBAMkuu wa Mkoa wa NJOMBE CHRISTOPHER OLE SENDEKA ameagiza kuundwa kwa tume ya kuchunguza chanzo cha moto kilichotekeza mabweni mawili katika shule ya sekondari ya ITAMBA wilaya ya MAKETE mkoani humo.Moto huo ulizuka Jumanne wiki hii katika shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kusini Magharibi umesababisha hasara ya zaidi milioni 80 na zaidi ya wanafunzi wa kike 70 kukosa mahali pa kulala.OLE SENDEKA ametoa agizo hilo baada ya kutembelea katika shule hiyo na kuahidi kutoa shilingi milioni MBILI ili kuwasaidia wanafunzi kupata baadhi ya mahitaji.Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari ITAMBA, DAUDI TUKINGE amesema moto huo umesababisha wanafunzi watano kulazwa hospitali baada ya kupatwa na mshtuko na kwamba chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.