Update:

16 February 2017

Serikali yaahidi kutoa fedha kukamilisha ujenzi wa HalmashauriWaziri Mkuu KASSIM MAJALIWA ameihakikishia Halmashauri ya wilaya ya KITETO mkoani MANYARA kuwa Serikali itaendelea kutoa fedha za kukamilisha mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri hiyo unaosuasua kutokana na kuchelewa kupata fedha.Waziri Mkuu MAJALIWA ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa ofisi hiyo ambao hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni NNE ambao ukikamilisha utasogeza huduma karibu na wananchi.Katika hatua nyingine Waziri mkuu MAJALIWA amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya wilaya ya KITETO na kujionea hali ya huduma na kuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha vifaa tiba na dawa zinapatikana ili kuwaondolea usumbufu wagonjwa.Waziri mkuu KASSIM MAJALIWA anaendela na ziara yake mkoani MANYARA