Update:

03 February 2017

RC ARUSHA asitisha wafanyabiashara kunyang’anywa vibanda


Mkuu wa mkoa wa ARUSHA,MRISHO GAMBO,amesitisha mpango wa jiji la ARUSHA wa kuwanyang’anya vibanda wafanyabiashara wa stendi ndogo ya mabasi jijini humo hadi utaratibu mpya utakapopangwa ili kulinda maslahi kwa pande zote husika.

Gambo ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati akizungumza na Wafanyabiashara wadogo ambapo amesema jiji linapaswa kutengeneza utaratibu mzuri ili waliojenga vibanda waendelee kufanya biashara pamoja na mapato ya serikali yaendelee kupatikana.

Baada ya kauli hiyo kutolewa na Mkuu wa mkoa,baadhi ya wafanyabiashara,wameshukuru hatua ya serikali yakuruhusu kuendelea kufanya biashara wakati michakato mingine ikiendelea.

Jiji la ARUSHA limeingia makubaliano na wapangaji wajenzi kujenga maduka kwenye eneo hilo kwa makubaliano ya kuishi mika 10 pasipo kulipa kodi lakini tayari muda huo umeshapita.