Update:

27 February 2017

POLISI watakiwa kuwashirikisha viongozi wa vijiji katika oparesheni zao.Askari wa Jeshi la Polisi Wilayani BUKOMBE wametakiwa wanapofanya operesheni yeyote ile katika vijiji vya wilaya hiyo wawashirikishe viongozi wa kijiji ili kazi waliolenga kuifanya katika kijiji husika ifanyike kwa amani na utulivu.

Akizungumza katika baraza la madiwani iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya BUKOMBE Mkuu wa Wilaya JOSEPHAT MAGANGA amelitaka jeshi hilo kutowadharau viongozi wa vijiji kuepuka migongano baina ya wananchi na jeshi la polisi.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa GEITA MEJA JENERALI MSTAAFU EZEKIEL KYUNGA amezindua ujio wa magari mawili ya kubebea wagonjwa zitakazopelekwa katika vituo vya afya vya UYOVU na USHIROMBO zilizotolewa na serikali kupitia Shirila la Afya Duniani.