Update:

28 February 2017

Pimgamizi dhidi ya Mbunge LEMA laondolewaMwenyekiti wa kikao cha jopo la Majaji Watatu wa Mahakama ya Rufaa, kinachoendelea mkoani Arusha, Bernard Luanda, amehoji namna wanasheria wa serikali walivyotumia mahakama katika uendeshaji wa kesi ya mbunge wa Arusha MJINI, Godbless Lema.Akizungumza Mahakamani hapo mbele ya majaji wenzake Stella Mugasha na Jaji Kipenka Mussa, Luanda amesema hatua ya Mbunge Godbless Lema kushikiliwa kwa miezi Minne bila sababu za msingi ni kumnyima haki.


Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo –CHADEMA, FREEMAN MBOE amesema wanasubiri mahakama kuu kufanya maamuzi kuhusu kesi ya Mbunge GODBLESS LEMA.Ameongeza kuwa kupitia mwendendo wa kesi ya mbunge Lema wamepata hoja watakayoiwasilisha kama ajenda muhimu katika bunge lijalo.Kesi hiyo inatarajiwa kurudishwa mahakama kuu ambapo ndipo utakapotolewa uamuzi kuhusu dhamana ya mbunge huyo.