Update:

28 February 2017

Msako wa viroba kuanza rasmiSerikali imesema itafanya operesheni maalum dhidi ya uzalishaji, uingizaji, usambazaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki vya pombe kali maarufu kama viroba kuanzia Machi pili mwaka huu.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesema operesheni imefuatia agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la februari 16 mwaka huu wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku sita mkoani Manyara.Waziri Makamba amesema zoezi hilo lenye lengo la kulinda afya za wananchi, kuongeza pato la taifa na kutunza wa mazingira litasimamiwa na wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mikoa.Aidha Waziri Makamba amesema serikali inaandaa utaratibu wa kukomesha uzalishaji, uingizaji na utumiaji wa mifuko ya plastiki na kuwataka wazalishaji na waagizaji kujiandaaKatika hatua nyingine baadhi ya wasimamizi na wamiliki wa Baa jijini DSM wameiomba serikali iwaruhusu wamalizie shehena viroba katika maghala yao .