Update:

27 February 2017

Marufuku kuhamisha watumishi bila kuwalipa stahiliMkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai ameitaka halmashauri ya wilaya hiyo kuacha kuwahamisha watumishi wa Idara ya Afya bila kuwalipa stahili zao.


Akizungumza na Waganga, Wauguzi na Watumishi katika Hospitali ya Kinyonga Mjini Kivinje, Ngubiagai amesema wapo watumishi waliohamishwa tangu mwaka 2004 lakini hadi sasa bado hawajalipwa stahili zao.


Mkuu huyo wa Wilaya ya Kilwa pia ametaka ukusanyaji mapato kwa mfumo wa kielektroniki uharakishwe ili kudhibiti upotevu wa mapato.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo amesema hadi sasa wana mashine 25 zinazotumika kukusanya mapato katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na wanatarajia kuongeza mashine nyingine.