Update:

16 February 2017

JAPAN yasaini makubaliano ya ujenzi wa BASSBALLUbalozi wa JAPAN nchini umesaini makabaliano na chama cha mchezo wa BASSBALL nchini wa ujenzi wa uwanja wa mchezo huo wenye thamani ya shilingi Milioni 170 katika shule ya sekondari AZANIA jijini Dar es salaam.


Balozi JAPAN nchini TANZANIA MASAHARU YOSHIDA na mwenyekiti wa chama cha bassball nchini DR. AHMED MAKATA,wanasema ujenzi wa uwanja huo utasaidia kuleta mapinduzi ya kuendeleza mchezo huo nchini.


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo NAPE NNAUYE amesema, uwanja huo utasidia kuongeza wachezaji watakaoshiriki mashindano ya OLYMPIKI JAPAN mwaka 2020.


Waziri NAPE pia ametumia nafasi hiyo kutangaza azima ya serikali kurejesha maeneo ya wazi na viwanja vya michezo vilivyovamiwa na watu ili kuendeleza michezo nchini.


Ujenzi wa uwanja huo wa bassball utaanza mwezi machi na kumalizikia mwezi JULAI mwaka huu,na utakua chachu ya timu ya TANZANIA kufanya vyema katika mashindano ya OLYMPIKI yatakayofanyika JAPAN mwaka 2020.