Update:

03 February 2017

CAMEROON KUKIPIGA NA MISRI FAINALI YA AFCON, WAICHAPA GHANA BAO 2-0


Timu ya Taifa ya Cameroon imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yanaoendelea kufanyika kule nchini Gabon, baada ya kufunga timu ya Ghana goli 2-0 yaliyowekwa mikiani na Ngadeu Ngadjui (dakika ya 72) na Christian Bassogog (dakika ya 90). kwa matokeo hayo, Timu ya Cameroon itakutana na Timu ya Misri katika mchezo wa fainali utakachezwa Februari 5, 2016 katika dimba la Libreville, nchini Gabon.