Update:

26 January 2017

Wananchi ARUSHA waomba kuwekewa mpaka kati yao na HifadhiViongozi wa kata na vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Taifa ya ARUSHA wameiomba serikali kuwasaidia kuondoa utata wa mpaka baina ya hifadhi hiyo na vijiji vyao ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.


Viongozi hao wamesema hayo wilayani ARUMERU wakati wa kikao cha kujadili changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa uhakiki wa mipaka wa hifadhi hiyo baada ya kubainika baadhi ya vijiji vimeingia ndani ya hifadhi .

Mpima ardhi wa wilaya ya ARUMERU, SEVERIN LUAMBANO, amesema kuna mpaka unaoonyesha baadhi ya vijiji vimeingia ndani ya hifadhi ya ARUSHA lakini akabainisha kuwepo kwa mpaka mwingine unaoonyesha kuwa wananchi hao hawajaingia katika eneo la hifadhi.


Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya ARUSHA STERIA NDAGA amesema katika kikao hicho wamekubaliana kuainisha maeneo yenye utata ili yaweze kujadiliwa na kutolewa maamuzi katika kikao kijacho.

Credit:TBC