Update:

19 January 2017

Tetesi zinazomkumba Trump baada ya kuibuka mshindi wa uchaguzi Marekani

Kumekuwa na tetesi kumhusu Donald Trump ambaye atakuwa rais wa 45 wa Marekani baada ya siku chache .Kwa kawaida Marekani huwa na majivuno ya kuwa mfano bora zaidi na mfumo wa demokrasia,lakini wakati huu mfumo wake umedhihirisha kinyume .
Baadhi ya wachambuzi wamekosoa uchaguzi mkuu wa Marekani na kudokezea uwezekano kuwa kulikuwa na udanganyifu katika shughuli hiyo.Urusi tangu mwaka 1945 imekuwa adui wa Marekani ,imetuhumiwa kuchangia katika udanganyifu wa uchaguzi huo kupitia vyombo vya habari.
Habari kupitia vyombo vya habari zimeeneza taarifa zinazoonyesha Marekani kuwa nchi dhaifu isiyoweza kujitegemea hata katika matukio kama uchaguzi mkuu .
Katika dunia hii hamna serikali yoyote itayoonysha dunia kuwa mamlaka ya uongozi ni dhaifu.Cha kushangaza ni kuwa bado wanaendelea kutumia mamilioni ya dola kuonyesha dunia jinsi mamlaka hiyo ni daifu .Mashirika ya serikali ya Marekani miongoni mwao CIA pia wamesambaza taarifa zinazoashiria kuwa hakukuwa na usalama wa kutosha kuhakikisha kuwa shughuli ya uchaguzi ni salama bila udanganyifu.
Huku wafuasi wa chama cha Democrats na baadhi ya taasisi za serikali ya Marekani wanashughulika kuonyesha dunia dunia jinsi Marekani ipo hatar,ini Rais Mteule Donald Trump anatoa uhakikisho jinsi atafanya Marekani kuwa na nguvu zaidi na nchi yenye kuaminika zaidi.Hata hivyo la kusikitisha ni kuwa Marekani sasa kupitia vyombo vya habari inaendelea kuchafua jina la serikali mpya itakayoshika usukani.
Miaka mingi iliyopita hali kama hii iliwahi kutokea nchini Urusi.Nchi ya Urusi ilikumbwa na pigo kuu baada ya mfumo wa Komunisti kuanguka .Maadili ya Urusi yalikuwa yanaendelea kudidimia kwa ajili ya hadhi ya raia wake .
Baada ya kuanguka kwa utawala wa kikomunisti,Jeshi la Red Army la Urusi ambayo ilikuwa hadhi kuu ya Urusi na pia lilikuwa likiogopewa dunia nzima lilianza kuchafuliwa jina kupitia vyombo vya habari.
Muungano huo wa jeshi la Urusi lilidaiwa kujihusisha na ulanguzi wa silaha haramu  kupitia taarifa za vyombo vya habari.Hii iliathiri sana soko la silaha kutoka Urusi kiasi cha kuwa hata roketi ya Urusi iliuzwa kwa thamani ya dola 30 pekee .
Madaktari,walimu,familia za warusi na kina mama wakaanza kutoroka nchi ya ona kwenda katika mataifa mengine wakifanya kazi na kupewa mishahara duni ya kati ya dola 150 hadi dola 200.Nyumba nzuri zilizokuwa zimejengwa kwa kutumia ubunifu wa asili ya Urusi zenye thamani ya mamilioni ya dola lakini ziliuzwa kwa tahamni ya dola elfu 3 au mbili .
Kipindi hicho Urusi ilikuwa katika hali mbaya sana .
Lakini raia mmoja wa Urusi kwa jina la Sergey Putin akasimama siku moja na kusema kuwa atasimamisha Urusi tena na  kurudisha hadhi ya raia wa Urusi.Raia wa Urusi kwa mara ya kwanza wakapata matumain,i na kuanza kumuunga mkono .
Kwa kuona hivyo vyombo vya habari vilianza kuchafua jina la Putin kama vile sasa Trump anaharibiwa jina na vyombo vya habari sasa .
Hata hivyo Putin alifanikiwa kuwa rais wa Urusi lakini bado viongozi wa makundi ya majambazi ya mafia yaliendelea na shughuli zao kwa siri nchini humo.
Mwaka 2002 ambapo rais Recep Tayyıp Erdoğan alikuwa anaungwa mkono na halaiki ya wananchi wa Uturuki alishambuliwa kwa habari za uongo kumhusu kupitia taarifa za wanahabari kama anavyofanyiwa Trump sasa .Rais Erdoğan amesaidia katika kuifanya Uturuki kuheshimika katika uchumi mzuri na maendeleo .Ameweza kuleta mabadiliko katika uongozi na haki na kunufainisha wananchi.
Miaka 15 iliyopita kama vile Trump aliahidi ataleta uongozi wa kuaminika zaidi kisiasa na kuifanya Uturuki nchi yenye Utajiri na nguvu zaidi.Mwanzo kabisa alianza kwa kuondoa biashara nchini zlizokuwa hazijasajiliwa .Alianza kwa kuhakikisha kuwa usawa unazingatiwa kulingana na sheria .
Rais Erdoğan pia alihakikisha kuwa jeshi lake limekuwa jeshi la nguvu na kwa mafanikio katika historia ya Uturuki jeshi la Uturuki limeendelea kuwa lenye nguvu .
Katika historia viongozi wa mataifa kama Brazili Dilma Roussef ,Putin,Erdoğan na Trump wanaofanya jitihada kuleta mabadiliko mazuri katika nchi zao wamekumbwa na tetesi za uwongo dhidi yao sawa zinazosambazwa kupitia  vyombo vya habari .
Rais wa zamani wa Brazil Roussef aliyefanya bidii kuokoa nchi yake kutokana na uhaba wa mambo muhimu ya nchi na pia kupandisha hali ya uchumi nchini humo sasa anakabiliwa na mashtaka ya kushiriki rushwa .Roussef alikuwa anapigania kuwa na usawa wa kugawanywa kwa mali asili za nchi ili kupunguza umaskini nchini humo .
Raia wa Brazil hawajasismama na kiongozi wake nas asa maskini wanaendelea kuwa maskini huku matajiri wakiendelea kuwa matajiri .Sasa Donald Trump anawahakikishia wananchi wa Marekani kuwa atabadilisha mfumo bora zaidi wa serikali yake itakayo leta matumaini ya maisha bora zaidi.
Lakini swali kuu ni kuwa je wananchi wa Marekani wataweza kusimama pamoja na kiongozi wao kama wananchi wa Urusi na Uturuki,wataweza kufanya pamoja na rais mtarajiwa Trump?
Credit:TRT