Update:

19 January 2017

Tanzania: Tanzania kuanza kuchimba Uranium hivi karibuni

Tanzania imeendelea kuharakisha mipango ya kuchimba madini ya uranium katika eneo la mto wa Mkuju kwenye hifadhi ya wanyama pori ya Selous licha ya kuwepo na upinzani kutoka kwa wanaharakati wa kulinda mazingira.
Serikali imeagiza kampuni ya Mantra Tanzania Ltd kuanza uchimbaji ndani ya miaka miwili ili kuwezesha nchi hiyo kunufaika na mapato ya kigeni kutokana na mauzo.
Naibu waziri wa kawi na madini Medard Kalemani amesema uchimbaji wa madini hayo ungeanza April 2015 wakati leseni ilipotolewa.
Tanzania inatarajia kupata bei zuri ya madini hayokutokana na kwamba mahitaji yake yanaendelea kuongezeka.
Uranium hutumiwa kwenye vinu vya kuzalisha kawi ya nyuklia.