Update:

18 January 2017

TAARIFA KWA UMMA: MAOMBI YA NAFASI 1000 ZA MAFUNZO YA STADI ZA KUTENGENEZA VIATU


JAMHURI YA 
MUUNGANO WA TANZANIA 
OFISI YA WAZIRI MKUU
KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE 
ULEMAVU 
MAOMBI YA NAFASI 1000 ZA MAFUNZO 
YA STADI ZA KUTENGENEZA VIATU
1.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira,
Vijana na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) inatekeleza Programu ya
Kukuza Stadi za Kazi Nchini ya miaka mitano (2016 -2021) ambayo imelenga
kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu
ushindani katika soko la ajira. Hivyo, OWM-KVAU imeingia makubaliano na 

Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam
Kampasi ya Mwanza iliyo eneo la Ilemela Mwanza,
kutoa mafunzo ya stadi za kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi. Lengo ni
kuhakikisha nchi inakua na nguvu kazi ya kutosha yenye ujuzi unaohitajika
katika soko la ajira katika kutengeneza bidhaa za ngozi nchini. 

2.
Ofisi inapenda kutangaza nafasi 1,000 za
mafunzo yatakayoanza ifikapo tarehe 20 Februari, 2017 katika Taasisi ya
Teknolojia Dar es salaam Kampasi ya Mwanza. Vijana wa Kitanzania, wenye elimu
ya msingi na kuendelea na umri kati ya miaka 18 hadi 35 wanaopenda kujiunga na
mafunzo wawasilishe maombi yao kuanzia tarehe 22/ 01/2017 hadi 04/02/2017
yakiambatana na nyaraka zifuatazo: 

(i)     
Barua ya maombi yenye anuani kamili
ikiwa na namba za simu pamoja na barua pepe; 

(ii)     
Nakala
ya Cheti cha Elimu uliyohitimu 

(iii)      
Nakala
ya cheti cha kuzaliwa au kadi ya mpiga kura; 

(iv)     
Barua  ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa
anaoishi mwombaji; na 

(v)     
Picha
nne za paspoti. 

3.
Maombi yawasilishwe kwa Mkuu wa Kampasi,
TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM – KAMPASI YA MWANZA, S.L.P.
2525, Mwanza au kwa barua pepe: info@mwanzacampus.dit.ac.tz 

4. Watakao kuwa na sifa na vigezo wataitwa

kwenye usaili kuanzia tarehe 8 hadi 11 Februari, 2017. 

IMETOLEWA NA: 

KATIBU MKUU