Update:

19 January 2017

Refa Mike Dean ashushwa daraja kutokana na maamuzi yake mabovu ligi ya EPLRefa Mike Dean amepewa adhabu ya kushushwa daraja hadi ligi daraja la kwanza kutokana na kutoa maamuzi mabovu kwenye baadhi ya michezo aliyowahi kuchezesha kwenye mechi za ligi kuu ya Uingereza. Mara kadhaa refa huyo amekuwa akilalamikiwa kuwa na maamuzi mabovu katika mechi anazochezesha. Mechi ambazo Dean analalamikiwa kuzitolea maamuzi mabovu ni ile ya West Ham United dhidi ya Manchester United baada ya kumpa kadi nyekundu kimakosa Sofiane Feghouli pamoja na kukubali goli la kuotea la Zlatan Ibrahimovic.

Mechi nyingine anazolalamikiwa ni pamoja na Everton dhidi ya Liverpool iliyochezwa Disemba 19 mwaka jana ambapo alionekana kuibeba zaidi Everton kutokana na kushindwa kutoa kadi nyekundu kwa Ross Barkley baada ya kumchezea rafu mbaya Jordan Henderson.

Mechi nyinyine ambazo aliharibu refa huyo ni Tottenham dhidi ya Aston Villa na Stock City dhidi ya Sunderland. Dean ambaye amechezesha mechi za ligi kuu kwa misimu 17 atachezesha mechi yake ya kwanza ya Championship Jumamosi hii watakapokutana mahasimu kati ya Barnsley dhidi ya Leeds.