Update:

27 January 2017

RC KILIMANJARO aagiza ujenzi wa Maabara kukamilishwaMkuu wa mkoa wa KILIMANJARO, SAID MECK SADICK ameelezea kusikitishwa kwake na kitendo cha viongozi wa kata ya KIA wilayani HAI kushindwa kukamilisha ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya KIA.

Akikagua miradi ya Programu ya maendeleo ya Shule za sekondari –SEDEP wilayani humo SADICK amesema inasikitisha kuona uongozi huo umeshindwa kuchangisha shilingi millioni moja na laki tano kwa ajili ya kumlipa fundi ili kumaliza ujenzi huo.

Kufuatia hali hiyo ameuagiza uongozi wa kata kuhakikisha maabara hiyo inakamilika haraka iwezekanavyo ili wanafunzi waweze kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi.

Akiwa wilayani HAI, Mkuu huyo wa mkoa wa KILIMANJARO pia amekagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na vyoo katika shule za sekondari KIA, KYUU na KIKAFU .