Update:

25 January 2017

Papa amtimua kiongozi wa dini kwa kusambaza kondomu


Kiongozi wa kanisa katoliki anayewasaidia raia wa Malta
amejiuzulu kufuatia mgogoro na Vatican kuhusu mpango wa kusambaza mipira ya
kondomu kulingana na kanisa hilo.

Mathew Festing mwenye umri wa miaka 67 alijiuzulu baada ya papa
Francis kumtaka kufanya hivyo katika mkutano siku ya Alhamisi. Hatua hiyo inafuatia ufichuzi kwamba tawi la hisani la kanisa
hilo huko Malta lilisambaza maelfu ya mipira ya kondomu katika taifa la
Myanmar.

Kanisa katoliki linakataza utumizi wa mipira ya kondomu. Papa Francis ilimtaka ajiuzulu na alikubali. Tawi hilo la Malta lina uwezo mwingi kama ule wa taifa zima.
Hutoa pasipoti, stampu na leseni na pia lina uhusiano wa kidiplomasia na
mataifa 106 ,ikiwemo Vatican.

Ijapokuwa tawi hilo linaonekana kuwa na wanaume pekee, viongozi
wake sio wanaume pekee.Kufikia 2013 wanawake walikuwa asilimia 30 wakijulikana kama
Dames.Kundi hilo lilo katika kuondoa sura yake ya kibwenyenye na
kuvutia vipaji ili kuendelea kazi zake za kibinaadamu.

Chanzo:BC


Papa Francis akiwa na kiongozi wa
kanisa katoliki anayewasaidia raia wa Malta