Update:

25 January 2017

MOTO WAZUKA KATIKA MOJA YA JENGO LA POLISI MKOANI KILIMANJARO USIKU WA KUAMKIA LEO, ZAIDI YA FAMILIA ZA ASKARI 20 ZAKOSA MAKAZI

Moto umezuka katika moja ya jengo la ghorofa mbili ambalo ni makazi ya askari Polisi, Moshi mkoani Kilimanjaro usiku huu na kuteketeza baadhi ya vyumba na Mali za familia za askari waliokuwa wakiishi katika jengo hilo.

Moto huo unadaiwa unaodaiwa kuanza kuwaka majira ya saa mbili za usiku, umepelekea zaidi ya familia za askari 20 kukosa makazi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, wamemedai kuwa chanzo cha moto huo huenda kikawa ni mshumaa uliokuwa ukiwaka katika moja ya vyumba hivyo kufuatia kukatika kwa umeme.


Moto ulipokuwa ukiendelea kuwaka katika Jengo hilo, kabla vikosi vya Zimamoto na Uokoaji kufika katika eneo la tukio.Sehemu ya Familia za Askari waliokuwa wakikaa katika Jengo hilo pamoja na mashuhuda wakiangalia tukio hilo wakati vikosi vya Zimamoto na Uokoaji vikiendelea na jitihada za kuudhibiti moto huo.Sehemu ya mali zilizoteketea kwa moto huo.