Update:

19 January 2017

Mchezaji wa zamani wa Misri Mohamed Aboutrika awekwa kwenye orodha ya magaidiMwanasheria Mohamed Osman, wa mchezaji wa zamani wa soka wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Aboutrika amesema Mamlaka za usalama za Egypt zimemweka mchezaji huyo katika orodha ya magaidi baada ya kuhusishwa na kikundi cha waislam wa Brotherhood. Bw. Aboutrika anashutumiwa kuwasaidia kifedha kikundi cha Brotherhood, kikundi ambacho mamlaka za Misri kimekiweka kwenye kundi la magaidi.

Kwa sheria za Misri, mtu yoyote anayewekwa kwenye orodha ya ugaidi, hufungiwa kusafiri na passport yake pamoja na mali zake hushikiliwa.

Kiungo huyo wa zamani wa Al-Ahly na timu ya taifa ya Misri, alikuwa kipenzi cha wananchi wa Misri na walifikia hatua ya kumpa majina ya The Prince of Hearts, The Magician na The Saint wakati akicheza soka, lakini uamuzi wake wa kumunga mkono Mohammed Morsi, ambaye alikaa madarakani kwa mwaka mmoja tu, uliwagawa mashabiki zake. Mwaka 2015, mali zake nyingi ziliwekwa kizuizini.