Update:

22 January 2017

Matokeo ya Uchaguzi Jimbo la DimaniMsimamizi wa uchaguzi mdogo wilaya ya magharib B Unguja jimbo la Damani Bi Fatma Gharib Haji amemtangaza Bwana Juma Ali Juma wa CCM kuwa mshindi halali katika nafasi ya ubunge jimbo la Dimani kwa kupata kura 4850 huku mpinzani wake kutoka Chama cha wananchi CUF Abdullrazak Khatib Ramadhani akipata kura 1234.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo na kura walizopata ni kama ifuatavyo:


Hamad Mussa Yusssuf (ACT) amepata kura 8
Issa Abdurahim Abdulkadir (ADC) amepata kura 42
Abdalla Kombo Khamis (Chauma) amepata kura 30
Magwira Peter Agathon (DP) amepata kura 8
Ali Khamis Abdalla (NRA) amepata kura 1
Amour Haji Ali (SAU) amepata kura 4
Pand Haji Pandu (TLP) amepata kura 2
Abdlsamad Salum Ali (UMD) amepata kura 2
Bakari Ali Omara (UPDP) amepata kura 1