Update:

19 January 2017

MADHARA YA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZA KIKE NA SULUHISHO LAKE.

Kwanza napenda kuwashukuru wote mnaofatilia masomo yangu, kama unavutiwa basi share na wenzako kisha kama una chochote basi usisite tuandikie kwa namba 0654 361 333
whatsapp/text.
Napenda niseme tu kwamba moja ya sababu kubwa iliyonigusa kuandika elimu hii juu ya kuvurugika kwa homoni za kike ambazo ni estrogen,progesterone, Follicle Stimulating Homon,Luteinazing Hormon na Testotestorone.
Kwani tatizo hili limekuwa ni tatizo ambalo kila mwanamke analo na wengi wao wametumia kila mbinu ya kuondoa tatizo na wameshindwa. 

Basi leo utajifunza jinsi gani unavyohangaika kuangamiza sisimizi kwa kutumia bunduki na ni uharibifu wa miundo mbinu katika uhalisia kwani hukuzaliwa na matatizo hayo, ulikuwa mwenye afya tele na unayefurahia hedhi yako bila tatizo.
MAMBO YANAYO ASHIRIA UNA TATIZO KATIKA HOMONI ZAKO ZA KIKE 
1. Kuwa na hedhi ya muda mrefu Zaidi ya siku 7 unatumia Zaidi ya pedi 2
2. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na maumivu Makali sana
3. Kuwa na hedhi yenye kuambatana na kichefu chefu,kuharisha
 4. Kuwa na hedhi iliyojaa woga mkubwa sana
5. Kuwa na hedhi ambayo haina mpangilio, Unaweza kuingia mara tatu kwa mwez mmoja, mara mbili au unaweza usipate kabisa hata miezi 6 hadi mwaka.
6. Kuwa na ndevu sehemu za usoni,kifuani nyingi kupita kiasi
7. Kuwa na kitambi cha tumbo la chini (Abdominal obesity) 
8. Kukosa mtoto kwa muda mrefu
9. Kukosa hamu ya tendo la ndoa lenye kuambatana na maumivu makali