Update:

17 January 2017

Lady Jaydee: Wanawake Wengi Wanaishi Katika Ndoa Zisizo na Afya kwa Uoga Wao.


Baada ya kufanikiwa kuingia kwenye mahusiano mapya ya kimapenzi na Spicy wa Nigeria, muimbaji mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Lady Jaydee amedai kuwa wanawake wengi ni waoga wa kuanza maisha mapya ya mahusiano.

Jaydee ambaye aliachana na mumewe Gadner G Habash ambaye alikuwa naye takribani miaka 13, amesema watu wengi wanapokuwa kwenye mahusiano kuna maisha wanakuwa wameyatengeneza, hivyo inakuwa ngumu kuondoka na kuyaacha.

“Wanawake wengi wanashindwa kutoka kwenye mahusiano, kwenye ndoa zisizo na afya ni kutokana na wao kutojiamini. Kwanza si jambo rahisi sana kama umekaa na mtu muda mrefu harafu uamue tu kuwa unaondoka. Kuna maisha ambayo mmejenga pamoja kwa hiyo unapoondoka unakwenda kuanza maisha mapya, watu wengi lile suala la kwenda kuanza maisha mapya ndiyo huwa wanaliogopa,”