Update:

19 January 2017

JIFUNZE KUWA NA MSIMAMO WA KUJIZUA KUPOTEZA MALENGO YAKO

Kuna wakati, Abunuwasi aliamua kuwa mfuga mbuzi. Alinunua mbuzi wa kufuga huku akiwa na lengo la kujiongezea kipato chake pindi mbuzi huyo atapoanza kuzaa, ili awafuge ndama wawe wengi na kumuwezesha kuwa tajiri kuliko wote waliokuwepo katika mji ule..

Siku moja Abunuwasi akipokuwa anampeleka mbuzi wake malishoni, alikuta kiatu kimoja kizuri sana katikati ya njia. Alisimama na kukiangalia. Kiatu kilipendeza machoni mwake ila akasema "kiatu hiki ni kizuri lakini mbona kipo kimoja tu?" Alitafuta kiatu cha pili pembezoni mwa njia ila hakukiona. Alipoona hawezi kuvaa kiatu kimoja, aliamua kukiacha palepale. .

Abunuasi akachukuwa mbuzi wake na mbele kidogo akaona kile kiatu cha mguu wa pili. Abunuwas alishangaa na akaona bora angelikichukua kile cha mwanzo kwa sababu cha pili kimepatikana.

Aliporudi pale mwanzo kukitafuta alichokiacha awali lakini hakukikuta tena, alijaribu kukitafuta lakini hakukiona. Basi akadhani kuna mtu amekiokota. Akarudi haraka alipomfunga mbuzi wake nako pia hakumkuta mbuzi wala kile kiatu kimoja. Mwisho akawa amemkosa mbuzi na viatu, Ndoto zote za Abunuwasi kupata utajiri zikaruka na akabaki na umasikini wake kwa sababu ya tamaa yake.
NI RAHISI MNO KUSHINDWA KUFANIKIWA KATIKA MIPANGO YETU ENDAPO..HATUWEKI AKILI YETU KATIKA JAMBO MOJA.
WENGI HATUTOFAUTIANI NA ABUNUASI..TUNAANZA JAMBO MOJA...GHAFLA LINATOKEA LINGINE..UNAACHA UNAANZA LINGINE..MWISHO UNAKOSA YOTE.
WEKA MACHO YAKO PAMOJA..KUWA NA STAMINA YA KUJIZUA KUPOTEZA FOCUS
Credit: Adson Kagiye