Update:

19 January 2017

Jengo laporomoka baada ya kushika moto mjini Tehran

Jengo la ghorofa 15 limeripotiwa kushika moto na kuporomoka mjini Tehran nchini Iran

Watu kadhaa miongoni mwao timu ya wazima moto wamenaswa katika jengo hilo lililoporomoka.
Jengo hilo linatambulika kuwa la masuala mengi ya kibiashara nchini humo.
Taarifa zafahamisha kuwa moto huo ulianza siku ya Alhamis katika mojawapo ya vyumba vilivyoko katika ghorofa ya 15.
Wazima moto waliowasili katika eneo hilo kuzima moto wameripotiwa kunaswa katika jengo hilo baada ya kuzima moto .
Hata hivyo chanzo cha moto huo bado hakijulikani.
Aidha idadi ya waliopo ndani ya jengo hilo lililoporomoka bado haijulikani.