Update:

27 January 2017

BARCLAYS yaanzisha shindano kwa wanachuo


Benki ya BARCLAYS imezindua mpango wa kupata wajasiriamali wenye michanganuo bora ya biashara kutoka vyuo vikuu nchini unajulikana kama University Enterpreneurship challenge ambao watapelekwa ujerumani kushindanishwa

Mratibu wa mpango huo VICTOR MNYAWAMI amesema wanachuo hao watatuma maombi yao kwa mtandao ambapo baada ya mchujo washindi wataingia katika mashindano mengine nchini UJERUMANI ifikapo mwezi Mei mwaka huu.

Naye msemaji wa benki ya BARCLAYS HELLEN SIRIA amesema kwa kudhamini shindano hilo benki yao inahamasisha ubunifu wa wanafunzi wa vyuo ili wakipatiwa mitaji waweze kuwa wajasiriamali wanaojiajiri wenyewe.