Update:

20 December 2016

LUKUVI AMTUMBUA MPIMA ARDHI WA MANISPAA YA MUSOMA


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amemuondoa Mpima Ardhi wa manispaa ya Musoma Mkoani Mara Bwana John Kapera na Kumtaka Katibu Tawala wa mkoa wa Mara amuondoe katika kituo chake cha kazi kuanzia kesho. 

 Bwana John Kapera amekuwa anasababisha matatizo mengi katika Manispaa hiyo na kupelekea kuwa kero kwa wananchi wa Musoma katika kupima ardhi na kumilikisha.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.