Update:

16 December 2016

Luis Suarez kujifunga Barcelona mpaka 2021

Mpaka sasa Suarez amefunga magoli tisa La Liga
Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez amekubali kusaini mkataba mpya na vigogo hao wa soka nchini Uhispania unaofikia thamani ya Euro milioni 167 ikijumuisha kipengele cha kumuuza kwa timu itakayomuhitaji.
Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool amefunga magoli 97 na kushinda vikombe nane tokea alipohamia Nou Camp Julai 2014 kwa ada ya Paundi milioni 75.
Taarifa kutoka Barcelona zinasema kuwa mkataba huo utakaomfunga Suarez mwenye miaka 29 mpaka mwaka 2021 utasainiwa siku ya Ijumaa.
Alifunga magoli 40 kwenye ligi kuu soka nchini Uhispania msimu uliopita.
Mshambuliaji mwingine Lionel Messi raia wa Argentina mwenye miaka 29 ana mkataba na klabu ya Barcelona mpaka mwezi June 2018 lakini mazungumzo ya mkata mpya tiyari yameanza.