Update:

16 December 2016

DAWA YA KUKATA HARUFU MBAYA YA KWAPA.

Wakisema watamke mwanamke mrembo hawataacha kutamka usafi ndani yake, usafi na usafi unahitajika kwa mwili wote, sasa leo tuone hiki kisehemu kidogo, lakini kikiamua kutoa harufu, kinakufukuzia mpaka marafiki, (KWAPA) Wanawake wengi tumekuwa tukioga, tunapulizia perfume kwenye makwapa kwa wale wenye uwezo, ili mwakwapa yasitoe harufu, lakini utakuta pamoja na kupulizia perfum bado sehemu ya kwapa inaacha alama ya njano, teyari inapunguza urembo wako, mtu akikuona atajua kabisa wewe ni mchafu.

wengine wansema kuwa ni Ugonjwa, uende hospitali, lakini kuna  dawa simpe na ni nzuri kwa kukata harufu, ni dawa ambayo hata mtu mwenye uwezo wa chini anaweza kununua, ni LIMAO AU NDIMU,
sasa leo mimi ninafahamu jinsi ya kutoa harufu ya kwapani bila kutumia perfumu,

1. unaoga unajikausha na taulo safi hasa makwapani,

2. unachukuwa Ndimu au Limao unakamulia kwenye mkono

3. unachukuwa yale majimaji ya ndimu unaanza kupaka kwenye kwapa,

kipingi cha kutumia limao /Ndimu pekeyake, huruhusiwi kutumia perfumu yeyote ile

unafanya hivyo kutwa mara mbili, asubuhi na jioni, na kwa wale wanaotoa harufu sana, basi wafanye hata mara tatu,

USISUGUE, itakuchubua, unapaka taratibu tu! wajaribu kwa muda wa siku tatu mfurulizo wataona mabadiliko na mashati hayataweka alama ya njano tena.

hapa hatumaanishi kwamba tusitumie perfume, maana nazo zina raha yake, zinafanya unukie vizuri sana,
ila kuna wale wenzetu ambao wanatoa jasho sana, kiasi kwamba imekuwa kero hata kwao, waweza tumia malimao kukata harufu hiyo, then ukishajiona uko okey, basi utaendelea kutumia perfumu,
Kwa maelezo na Ushauri kutana na Dr.Emmanuel Mabisi. +255782728971