Update:

16 December 2016

Darassa :''Sina Ugomvi na Saida Karoli


Mwanamuziki wa muziki wa kufokafoka (Hip Pop) nchini, Darasa amekana kuwa yeye amewahi kukutana na msanii wa muziki wa asili utoka mkoani Kagera, Saida Karoli na kuzungumza nae biashara yoyote ya muziki.

Darasa amesema hayo alipokuwa akizungumza na kituo kimoja cha habari hapa nchini na kusema wimbo wake sio wa midundo ya Saida Karoli bali ni midundo ya kitamaduni la kabila la kihaya.

“Midundo ya ngoma ya "Muziki" na ya Saida Karoli ni vitu viwili tofauti kabisa. Mtayarishaji wangu Abba kapiga kwa hisia zake lakini mtu mmoja akasema kwanini tusimshirikishe saida karoli kwa kuwa yeye ni mtu wa huko huko lakini hilo alikufanikiwa” Amesema Darasa.

Amesema kuwa mtu anatakiwa kuchukua midundo ya Saida karoli na kusikiliza marimba yaliyopigwa katika wimbo wangu wa "Muziki" na kuona tofauti.

Ameongeza kuwa mara baada Diamond kutoa wimbo wa "Salome" ndipo wazo la kumshirikisha Saida Karoli likafa. Hivyo ndio akajitokeza Ben Paul na yeye kama msanii mkubwa kaamua kuitendea haki nyimbo ndio mnaona leo baraka za nyimbo hiyo kukubarika na kila mtu.

Amemaliza kwa kusema kuwa anamshukuru mungu kwa kuwezesha wimbo huo kupenya kila mahali hasa kwa kuvunja rekodi kwa kuwa wimbo wa kwanza wa muziki wa kufokafoka kuweza kuchezwa mpaka kwenye Kitchen Party.