Update:

03 November 2016

UN yauchagua mji wa Al-Ahsa kuwa mji wenye ubunifu zaidi duniani


Umoja wa Mataifa wachagua mji wa AL Ahsa unaopatikana mashariki mwa Saudi Arabia kuwa mji wenye ubunifu zaidi duniani siku ya miji Duniani.
Mnamo Oktoba 31 mwaka 2014 Umoja Wa Mataifa ulizindua siku maalum ya miji duniani ili kuhamasisha ufahamu kuhusu ukuaji wa miji na jinsi ya haja ya ushirikiano katika changamoto zinazotokana na ukuaji wa miji na uchumi.
Asilimia 54 ya watu wote duniani huishi mijini na inakadiriwa kuwa itapanda na kuwa asilimia 66 ifikapo mwaka 2050.