Update:

05 November 2016

Sudan Kusini kwenye hatari ya kukumbwa na njaa

Mzozo unaoendelea nchini Sudan Kusini huenda ukachangia kushuhudiwa kwa baa la njaa wakati watu wanaendelea kukimbia makwao na kuacha mazao yao yakioza mashambani, kwa mujibu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP.
Kulingana na WFP hadi watu milioni 4 hawana usalama wa chakula.
Utapiamlo umepita asimia 15 kwenye majimbi Saba kati ya majimbo kumi ambapo majimbo ya Unity na Bahr el Ghazal yameathirika zaidi
Zaidi ya watu milioni moja wameihama nchi hiyo huku watu 4,000 wakivuka na kuingia Uganda kila siku