Update:

04 November 2016

Kipa wa Gambia afariki kwenye msafara wa wahamiaji haramu

Kipa wa timu ya taifa ya Gambia Fatim Jawara ameripotiwa kupoteza maisha alipokuwa akijaribu kukimbilia Ulaya kwenye mashua ya wahamiaji haramu.
Mashua hiyo ya wahamiaji haramu ilizama kwenye pwani ya Libya baada ya kukumbwa na misukosuko ya baharini wakati wa msafara wa kuelekea Ulaya.
Shirikisho la kandanda la Gambia limetoa maelezo na kutangaza kufariki kwa Jawara mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni kipa wa timu ya taifa ya wanawake.
Rais wa shirikisho la kandanda la Gambia Lamin Kaba Bajo alituma salamu za rambirambi kwa familia ya Jawara.