Update:

08 November 2016

Baada ya Lema kukaa mahabusu siku saba, leo amefikishwa mahakamani

Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema ambaye alishtakiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya viongozi wa serikali, leo November 8 amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Arusha na kusomewa shtaka linalomkabili baada ya kukaa mahabusu kwa siku saba.
Hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi anayesikiliza kesi hiyo Desdery Kamugisha amesema hawezi kutolea maamuzi kwenye mahakama hiyo kwa kuwa anahitaji muda wakusoma na kupitia vifungu vya sheria na hoja zilizotolewa na November 11 atatoa maamuzi.
Kutokana na hatua hiyo Godbless Lema amerudishwa rumande hadi November 11 mwaka huu. Wakili wa Chadema John Malya amesema kutokana na hoja zote zilizowasilishwa kwa pande zote mbili zimeonekana zina uzito hivyo wanasubiri uamuzi wa mahakama.
Source: millardayo.com