Update:

22 October 2016

Sharti ya upandaji miti kwa wanafunzi nchini Tanzania

Kwanzia mwaka 2017,wanafunzi wanaoanza shule ya msingi na upili watatakiwa si kubeba vitabu pekee bali pia na miche ya miti nchini Tanzania .
Sheria hiyo mpya ilitangazwa na waziri wa mazingira nchini humo January Makamba kama mpango mpya kwa serikali ya Tanzania katika jitihada za kulinda mazingira .
Waziri Makamba alisema kuwa wanafunzi hao watatakiwa kutunza miti hiyo hadi wanapohitimu na itakuwa moja ya mambo yatakayochangia katika kupeana kwa vyeti vya kuhitimu .
Aidha waziri huyo pia alifahamisha kuwa atawasilisha agizo hilo kwa halmashauri zote za mitaa na wizara ya Elimu .
Nchini Tanzania watoto hujiunga darasa la kwanza wakiwa na umri wa miaka 7 na kuhitimu wakiwa darasa la saba
sourse:trt swahili