Update:

21 October 2016

Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zasaini makubaliano kuhimiza biashara ya kuvuka mpaka

Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimesaini makubaliano ya biashara kusameheana ushuru wa forodha ambayo yanalenga kukuza biashara kati ya kuvuka mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Makubaliano yataondoa vizuizi visivyo vya lazima mpakani kwa biashara kati ya nchi hizo mbili. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, nchi hizo zimekubaliana kuhusu orodha ya bidhaa 168 zinazosamehewa ushuru wa forodha usiozidi dola za kimarekani 2,000.
Waziri wa biashara na viwanda wa Rwanda Bw. Francois Kanimba amesema hii ni hatua mpya kwa wafanyabiashara wadogowadogo wa nchi hizo mbili kufanya biashara kwa uhuru bila ya vizuizi.