Update:

21 October 2016

Ndege sita kubwa kutua na Mfalme wa Morocco Oktoba 23

NDEGE sita kufunika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius K. Nyerere katika ujio wa Mfalme wa Morocco Mohamed Vi akiongozana na wafanyabiashara 1000.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ziara hiyo ina manufaa kwa watanzania hivyo fursa ambazo zinaibuliwa kutokana ujio viongozi mbalimbali zitumiwe vizuri katika kujiletea manufaa.

Amesema kuwa ujio huo wa Mfalme wa Morocco utakwenda sambasamba na kusaini baadhi ya mikataba 11 kwa ikiwemo ya mahusiano, Reli ya Mchuchuma na Liganga, Uvuvi, Kilimo, utalii, siasa na mahusiano.

"Rais Dk. John Pombe Magufuli amekuwa akifanya kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania hivyo kila mtu atumie fursa hiyo kwa vitu vitakavyoibuliwa"Amesema Makonda.

Kutokana na ujio huo, watanzania wametakiwa kwenda kuulaki ujio wa kiongozi huyo ikiwa ni kuonyesha ukarimu wetu wenye amani.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema Mfalme wa Morocco atazindua jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti Bakwata.

Katika ziara hiyo wafanyabiashara watanzania watakutana na wafanyabiashara wa Morocco na kujifunza jinsi ya kushirikiana kibiashara kwa maendeleo ya taifa.
Ziara hiyo inatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 27 na kuondoka nchini saa 10 jioni