Update:

12 October 2016

Matokeo ya mechi za kufuzu kombe la dunia la FIFA 2018

Ujerumani, Poland zawika nyumbani kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia la FIFA 2018

Michuano ya kuwania nafasi ya kufuzu kwenye mashindano ya kombe la dunia la FIFA 2018 iliendelea hapo jana ambapo makundi 3 ya C,E na F yalicheza.
Ujerumani iliikaribisha Northern Ireland na kuondoka na ushindi wa 2-0 uliochangiwa kwa magoli yaliyofungwa na Julian Draxler katika dakika ya 13 na Sami Khedira katika dakika ya 17.
Kwingineko Poland iliilaza Armenia 2-1 kwenye mechi yao waliyocheza nyumbani.
Matokeo kamili ya mechi zote zilizochezwa hapo jana ni kama ifuatavyo;

Kundi C:

Ujerumani - Northern Ireland: 2-0
Czech Republic - Azerbaijan: 0-0
Norway - San Marino: 4-1

Kundi E:

Kazakhistan - Romania: 0-0
Denmark - Montenegro: 0-1
Poland - Armenia: 2-1

Kundi F:

Slovenia - Uingereza: 0-0
Slovakia - Scotland: 3-0
Lithuania - Malta: 2-0