Update:

20 October 2016

ARUSHA:MWENYEKITI AMKATA MWANANCHI KWA JEMBE KICHWANI KISA MAJI YA MFEREJI

mwekiti wa mtaa  olikeriani katika kata  ya moshono amemlima na jembe kichwani mwananchi wa  mtaa wa wake  kwa ugomvi wa maji ya mfereji  kwa ajli ya kunyeshea mazao mbalimbali
akizungumza na sunrise radio mhanga wa tukio hilo la kupigwa na jembe la kichwa bwana daniely longilu amesema kuwa mwenyekiti  huyo alimkuta ananyeshea shamba lake na katika mabishano akanyanyua jembe na  kumpiga la kichwa kisa yeye ana dhamana ya mwenyekiti  kwani maji ilikuwa si zamu yake ila mwenyekiti alichukua kimabavu
kwa upande wake shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mkazi wa eneo hilo amesema kuwa ni kawaida ya yake mwenyekiti wa huyo kupiga watu na kutochukuliwa hutua  yeyote kwani maji isiwe sababu ya kutoa uhai wa mtu
katibu wa chama cha ccm kata ya mshono bwana meshaki  laiboni kivuyo amesema kuwa  wananchi wamesikitishwa na  tukio hilo la mwenyekiti kumlima mwananchi jembe la kichwa  wakati mwenyekiti anatakiwa asimamie ulinzi na amani kwa wananchi wake ila yeye ndo kanza kuvunja amani  kwa wananchi
Imeandikwa na Praygod Martin