Update:

13 September 2016

ZIJUE DALILI ZA MAGONJWA YAZINAAKijana uonapo dalili moja, au zaidi kati ya hizi zifuatazo nenda kwenye kituo cha huduma ya afya kwa uchunguzi;
Kwa kijana wa kike
• Maumivu chini ya kitovu
• Kutokwa na usaha au majimaji yenye harufu mbaya
sehemu za siri (angalia picha)
• Kuwashwa sehemu za siri
• Vidonda na vipele sehemu za siri, mdomoni na sehemu nyingine za mwili
• Maumivu wakati wa kujamiiana
• Kuvimba mitoki
• Kuota sundosundo sehemu za siri
• Kukojoa mara kwa mara kunakoambatana na muwasho au maumivu

Kwa kijana wa kiume:
• Maumivu makali sehemu za siri wakati wa kukojoa
• Kutokwa na usaha sehemu za siri
• Vidonda sehemu za siri Vidonda sehemu za mdomoni Kuvimba mitoki
• Kupata malengelenge
• Kuota sundosundo (warts) sehemu za siri
Baadhi ya tabia ambazo zinaweza kuchochea kupata maambukizi ya magonjwa ya ngono kwa urahisi zaidi:
• Kujamiiana bila kondomu-vijana wengi hukosa
ujasiri wa kusisitiza matumizi ya kondomu kwa kuhofia kuachwa na wenzi wao
• Kujihusisha na ukahaba
• Kujamiina na wapenzi wengi
• Kunyonyana sehemu za siri-kwa kuwa vimelea vya magonjwa ya ngono vinapatikana kwenye majimaji ya sehemu za siri ni rahisi mtu mwenye maambukizi ya magonjwa ya ngono kumwambukiza mwenzi wakati wa kunyonyana.
• Kunyonyana ndimi (kula denda)-baadhi ya vimelea vya magonjwa ya ngono hupatikana mdomoni(Kisonono, Kaswende naVirusi vya UKIMWI) hivyo
huambukiza kupitia kunyonyana ndimi ikiwa mmojawapo ana maambukizi.
• Woga wa vijana wa kike kuwashawishi vijana wa
kiume kutumia kondom wakati wa kujamiiana kwa sababu ya mfumo dume.
• Kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazosababisha
kufanya ngono bila mpangilio, kwa mfano; makundi yanayoenda ufukweni, kuangalia filamu za ngono au kushiriki kwenye ngoma za jadi zinazochezwa
usiku kucha, disko na matamasha
• Kuhusika na vitendo vya ubakaji
• Utumiaji wa madawa ya kulevya au pombe ambayo
husababisha kijana kukosa ufahamu na hivyo kufanya ngono isiyo salama.
By Dr. Emmanuel John Mabisi