Update:

23 September 2016

VITAMBULISHO VYA TAIFA SASA NI ZAMU YA MTWARA

Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa limeendelea mkoani Mtwara, ambapo wananchi wamejitokeza kwa wingi kujisajili, hasa Wilaya za Tandahimba na Newala .

Pamoja na kujitokeza huko kwa wingi kwa watu, matatizo kadhaa yametishia kufanyika kwa ufanisi kwa suala hilo mkoani humo huku  wakazi wengi hususani maeneo ya vijijini kukosa mashine za photocopy, huku baadhi wakikosa nyaraka muhimu za kuwatambulisha vikionekana kuwa vikwazo zaidi.

Hata hivyo kwa maelekezo na mafunzo yaliyotolewa na NIDA kwa maafisa wote wanaoendesha zoezi hilo changamoto nyingi zimeweza kutatuliwa kutokana na miongozo na madodoso yanayomsaidia mwombaji kutambua baadhi ya taarifa muhimu.


NIDA imewaomba wananchi katika maeneo mengine ambayo zoezi hilo halijafanyika kuanza kujiandaa kwa kuwa na nyaraka muhimu zinazoweza kuwatambulisha mathalani; cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Cheti cha Elimu ya Msingi, Sekondari au Chuo, Leseni ya Udereva, Kadi ya kupigia Kura, Pasipoti, Kadi ya Bima ya Afya, nambari ya utambulisho ya mlipa kodi (TIN) pamoja na kuwa taarifa sahihi zinazomhusu mwombaji binafsi na wazazi, majina, tarehe na miaka ya kuzaliwa.