Update:

21 September 2016

Serikali sasa kupata kupata ufumbuzi wa tatizo soko la mbaazi mjini Babati

Wakulima wa  zao la mbaazi wamehakikishiwa kwamba tatizo la soko la  mbaazi limefika mwisho kwani serikali inafanya iwezalo ikiwemo kutangaza bei elekezi kwa wanunuzi wote mkoani Manyara.

Akizungumza na  wanunuzi wa zao hilo jana  mkuu wa mkoa waManyara Dkt Joel Bendera alisema bei ambayo ni elekezi kwa sasa ni shilingi 1200 kwa kilo moja.

Aidha  amewataka wanunuzi wote kufuata bei hiyo iliyoelekezwa na serikali wakati wa kikao cha maridhiano kilichofanyika ili kuweza kupanga bei hiyo kwa ajili ya kuweza kuwasaidia wakulima ambao tayari walikua waanza kuzitelekeza mbaazi mashambani.

Dkt  Bendera aliwatahadharisha wanunuzi ambao wanahusianisha bei ya mkoa huu na bei za mikoa mingine  jirani ambazo zimeguswa na wanunuzi hao huku akitamba kuwa mkoa wake ndio una mbaazi nyingi na nzuri.