Update:

29 September 2016

Rais Uhuru Kenyatta atuma ujumbe wa rambirambi kwa Israel kufuatia kifo cha Shimon Peres

Ujumbe wa rambirambi wa Kenyatta kwa Israel
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliungana na viongozi wengine duniani kufariji Israel na familia ya rais wa zamani wa Israel Shimon Peres aliyeaaga dunia mapema siku ya Jumatano.

Katika hotuba yake Kenyatta alielezea kuwa Peres alikuwa kiongozi kamili na mwenye nguvu aliyeongoza nchi yake kwa utofauti maalum.

Aidha alisema kuwa Peres atakumbukwa kuwa kiongozi aliyekuwa jasiri na pia mwenye aliyependa kuhamasisha amani.

“Israel imempoteza kiongozi muhimu,kwa niaba ya wannchi wa Kenya namuomba Mungu awape familia na Israel nguvu wakati huu mgumu.”

Shimon Peres amefariki akiwa na umri wa miaka 93,atakumbukwa kuwa waziri mkuu wa Israel mara tatu mfululizo na baadaye kuwa rais kati ya mwaka 2007 hadi 2014.

Peres pia aliwahi kuwa mshindi wa tuzo la amani mwaka 1994 .

Shimon amefariki hospitalini baada ya kulazwa akikumbana na maradhi ya kiharusi ambayo yalisababisha kutokwa na damu katika ubongo.