Update:

21 September 2016

MAJIKO YANAYO TUMIA NISHATI YA JUA KUZINDULIWA ROMBO

HALMASHAURI  ya Manispaa ya Alvis bin nchini Sweeden kwa kushirikiana na halmasauri ya wilaya ya Rombo zimeanza rasmi utekelezaji wa mradi wa hifadhi mazingira kwa kuzindua majiko yanayotumia nishati ya Jua.

Nishati hiyo ambayo inatumia karatasi za kufungia chakula (Foil paper) na kufungwa katika Dishi mithili ya linalotumika kupokea mawimbi ya sauti na picha katika ving'amuzi, itapunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa asilimia 80.

Kiongozi wa mradi kutoka Sweeden, Britt Hallerstrand amesema kuanza kwa mradi huo kunatanguliwa na mafunzo kuhusu ujasiriamali na utunzwaji wa mazingira uliototolewa kwa jamii tangu mwaka 2015.

Amesema nishati hiyo ambayo imefanyiwa majaribio nchini Sweeden na baadhi ya vijiji wilayani Rombo imeonesha mafanikio na hupika chakula kwa muda mfupi ikilinganishwa na nishati nyingine kama Kuni, Mkaa na Umeme.