Update:

15 September 2016

KWANINI WATU WENGI HAWATHUBUTU?

A.```Hofu ya wasichokijua (Fear of unknown)``` 
Hofu ndiyo sababu kubwa inayowafanya watu wengi wasiweka mawazo yao katika utekelezaji .Watu wanaogopa kupata hasara na kupoteza rasilimali nyingi sana ukiwemo muda.Hofu ambayo wao ndio wameitengeneza wenyewe imekwamisha mambo yao mengi sana na kushindwa kujua kuwa kitu pekee cha kuogopa chini ya jua ni hofu  na si vinginevyo .

B. ```Kuwa na tahadhari nyingi (too cautious)``` 
Tahadhari nyingi zimekuwa kikwazo za watu wengi kutofanikiwa kuweka mawazo yao katika utekelezaji .Wamekuwa wakiweka tahadhari nyingi kuliko kuona faida kubwa watakayoipata baada ya kuthubutu .Mbona wakati wa kuoa au kuolewa hukuweka tahadhari nyingi ???  .Mbona umeoa au kuolewa na mtu ambaye historia yake huuijui na hukuweka tahadhari nyingi kama unazoweka unapotaka kuanzisha vitu ??

C.```Urefushwaji wa muda(Procrastination)```✏Watu wengi huwa wana tabia ya kusema nitafanya kesho utadhani wana mkataba wa kudumu na Mungu kuwa ataishi milele .Hajui kuwa muda ni sasa na siyo kesho .
```Pastor Kelvin Kitaso``` mwandishi wa vitabu anasema : _“kinachowatofautisha watu waliofanikiwa na watu ambao bado hawajafanikiwa ni katika hali ya kuthubutu ,watu waliofanikiwa na wanaofanikiwa ni Watu wenye uthubutu wa kufanya mambo yao na hao hutawaliwa na neno *“NINA”* lakini  watu wasiofanikiwa mara zote huogopa kudhubutu na hutawaliwa na neno *“NITA”* .Siri kubwa ya mafanikio yetu kila siku IPO katika kuthubutu kufanya na si kuweka vipolo kwa visingizio kuwa nitafanya .Na kama usipothubutu kamwe huwezi ukafika unapohitaji kufika .Kama unataka kufika sehemu ni lazima uamue kuchukua hatua ya kufanya"__

D.```Watu waliowazunguka(Peer)```
Kama umezungukwa na watu ambao hawajawahi kuthubutu na hawana mpango wa kuthubutu  na wewe pia huwezi kuthubutu .Marafiki zako wanaokuzunguka wana mchango mkubwa wa kukufanya uanzishe vitu hata kama ni vidogo .Kumbuka vile ulivyo ni matokeo ya watu waliokuzunguka na si vinginevyo  na ndiyo maana zamani usipoonekana nyumbani mtu wa kwanza kuulizwa alikuwa rafiki yako wa karibu na si mdogo wako .Angalia sana umezungukwa na watu wa namna gani ili kufikia ndoto zako vinginevyo utaishia njiani maana usipoziba ufa utajenga ukuta.

E.```Ukosefu wa maarifa (Lack of knowledge)```
Watu wengi hawana maarifa ya maisha ambayo yanaweza kuwasaidia kubuni vitu vipya vyenye radha tofauti.Kwa kukosa maarifa watu wameshindwa kujua wataanzaje biashara au miradi migine kwa namna gani .Ukosefu wa maarifa umefanya watu kufikiri kuwa ili uanzishe kitu unahitaji mamilioni ya fedha kumbe kuna biashara inahitaji mtaji wa maarifa na biashara hiyo inafanyika kiurahisi ..```(Hivi kutoa ushauri wa kitaalamu kwa njia ya mtandao unahitaji dollar za kimarekani ngapi??? ).```

F.```Lawama (Blame):```
Hakuna jambo linalokwamisha maendeleo ya mtu kama lawama .Watu wanalaumu kuwa hawana mitaji ,watu wanalaumu familia zao na ndugu zao kwamba hawajawasaidia ,watu wanalaumu viwango vya elimu walivyo navyo na wamediriki kulaumu pia serikali kuwa haijawasaidia  na wamebaki tu bila kufanya chochote huku wakipoteza muda mwingi wakiwa wanalalamika vijiweni na huku wanakunywa kahawa na kusoma magezeti(sijui hela za kunywa kahawa na kununua magezeti ya michezo na udaku wanazipata wapi wakati wanasema hawana mitaji ).

G. ```Kushindwa kutumia fimbo iliyo mkononi:```
Watu wengi wanapenda kuanzia sehemu kubwa bila kujua kuwa fimbo iliyo mkononi ndiyo iuayo nyoka .Huhitaji mtaji wa milioni mia kuanza biashara ya genge .Huhitaji dola nyingi za kimarekani kuanzisha biashara ya chips .Fanya kile unachoweza kufanya kwa wakati huo.Nini unacho ?? una ujuzi ???  tumia ujuzi wako kubuni vitu ambavyo ukitumia ujuzi vitakuongezea hatua?? .Angalia ,Hakuna anayetembea huku miguu yote inaenda usawa mmoja ,lazima mguu mmoja uanze mguu mwingine utafuata kinyume na hapo kutembea hutaweza au utapata shida sana kutembea kama unataka miguu yote iende sawa .