Update:

23 August 2016

UVCCM: Tutaandamana kumpongeza Rais Magufuli

Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umetangaza kufanya maandamano nchi nzima Agosti 31 mwaka huu, ikiwa ni siku moja tu kabla ya tarehe iliyotangazwa na Chadema kufanya maandamano na mikutano nchi nzima.
UVCCM
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu amesema lengo la maandamano yao ni kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya tangu alipoingia madarakani.
“Maandamano yetu ni ya amani, na tayari tumeshatoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi kama taratibu zinavyotaka”,alisema.
Ikumbukwe kuwa kuna joto la vijana wa Chadema kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kwa walichodai kuwa wanataka kufanya oparesheni ya kupinga ukandamizwaji wa demokrasia nchini (UKUTA) na tayari jeshi la polisi Tanzania limeyakataza maandamano kama hayo.