Update:

30 August 2016

UNAPO KUWA UMEZUNGUKWA NA WATU HAWA KAMWE NI NGUMU KUFANIKIWA

Moja ya vitu ambavyo vimesababibisha watu kutofanikiwa ni kutokana na aina ya watu ambao wameamua kuambatana nao  .Wamesahau kuwa aina ya watu tunaoambatana nao wanamchango mkubwa katika maisha yetu ya kila siku na zaidi huathiri tabia zetu .
Mfano kwangu mimi sikuwahi kufikiria kuwa mwandishi lakini kumbe kitu hiki kilikuwa ndani yangu .Hata hivyo ni baada ya kuambatana na watu ambao ni waandishi kama *Kelvin Kitaso mwandishi wa kitabu Cha Getting prepared for Post-university life, Joseph Mayagila mwandishi wa Jinsi ya kuwa tajiri ,Adabert Chenche mwandishi wa kitabu cha Kwanini ufeli?,Adam Ngamange mwandishi wa kitabu cha Daraja ,Mabula jilala mwadishi wa Makala katika blog ya Morning Tanzania ,Edson Kashindi mwandishi jipukizi wa makala kwenye blog ya maisha na mafanikio*.
Unakumbuka kuwa hata *PETRO* moja ya wanafunzi wa *YESU* ilifikia hatua hata ongea yake,mwendo wake na mengine mengi alifanana na mwalimu wake hata kama yeye alikana kuwa siyo lakini ukweli ulikuwa uko pale pale .Hii ni kwa sababu muda mwingi alikuwa yuko na YESU.
Hawa ni watu ambao kama ndio unaambatana nao kamwe usitarajie muujiza wa kufanikiwa :
1. *Watu wenye mtazamo hasi*: Watu hawa ndio sumu kubwa katika mafanikio yako .Hawa ndio wale wanaona kila unachokiamini kuwa kinawezekana wao wanasema hakiwezekani .Watu hawa ni watu ambao huona pafupi sana wanafanana na mtu mwenye tatizo la kuona mbali ambaye usaidizi wa huyu mtu ni kumpa miwani ya lenzi mbonyeo  kumsaidia kuona mbali
Watu wenye mtazamo hasi wataangalia madhaifu yako kuliko uwezo wako na watakwambia hayo madhaifu kukufanya usisonge mbele.Watu hawa watakupa mifano mingi ya !Watu wenye mtazamo hasi wanaweza kuwa rafiki zako,ndugu zako ,mchumba wako ,mke wako ,majirani au mtu yeyeyote .
2. *Watu waoga*:  Adui mkubwa wa mafanikio ni kuwa mwoga na zaidi mwoga wa kitu usichokijua .Kuna watu ni waoga hata katika kufanya vitu vya maendeleo .Hawa ni watu ambao hupaswi kamwe kuambatana nao maana watakuambukiza uoga na hutakuwa mtu wa kujiamini .
Watu waoga ndio wale watu wenye tahadhari nyingi sana kabla ya kufanya vitu na mara nyingi wamekuwa hawafanyi kabisa mpaka wanaingia kaburini .
Jitahidi sana kuambatana na watu ambao hawatapanda mbegu ya kuogaopa kila kitu hata kama ni kitu cha maendeleo .
3. *Watu wambea*: Hili ndilo kundi kubwa la watanzania wengi ambao hutumia muda mwingi kujadili maisha ya watu huku wakisahau maisha yao .Ni kundi ambalo siku nzima huweza kuisha wakiwa wanamjadili mtu huku yule wanayemjadili akiwa anafanya yake kwa maendeleo yake wao wakiwa wanajitafuna wenyewe maana wanapoteza rasilimali muda ambayo ni rasilimali kubwa na ya muhimu .
Rose muhando mwimbaji nguli wa nyimbo za injili maarufu kama Malkia wa injili anasema watu wa jinsi hii hufuata jua ,jua likisogea nao wanasogea .
    *USHAURI*
*Ni muhimu sana kujua aina ya watu unaopaswa kuambatana nao .Naomba ieleweke kuwa watu wote tunapaswa kupendana lakini swala la kufuata kila wanachokisema na tabia zao zinahitaji utashi wa kuelewa aina za watu*