Update:

30 August 2016

Unajua kilichokatisha ndoto yako?

Kila mtu alipozaliwa aliingiwa na hamu /shauku ya kuwa mtu Fulani
Nakumbuka shule ya msingi tuliimba nyimbo za Nani tunatamani kuwa
kiu na hamu yako Ilikuwa sahihi Kabisa
Lakini Nini kimekatisha Ndoto zako??
Moja ya vitu ambavyo vimekatiza Ndoto zako ni kushindwa kujiuliza maswali haya ✍
1.Mimi ni nani?? : Watu wengi hawajielewi. Wanajua tu Majina yao Lakini hawajitambui wao ni akina nani. Jiuliza kila siku swali hili Sana. Je Wewe ndiwe Yule Mungu alikusudia kuwa???
2.Napaswa kufanya nini :hapa ndio sehemu ya kujua kusudi lako. Tafuta Sana kujua sehemu yako. sehemu yako Ipo ila hujaigundua. Umeangukia sehemu ambapo siyo sehemu yako kwasababu ya shida zako binafsi. Ndio maana hapo ulipo huna Furaha. unajivuta Hata kwenda kazini kwasababu Hiyo kazi siyo yako. Tumia muda wako kutafuta eneo lako .
Siri ni hii kwamba mara unapojua eneo lako hautakuwa bendera Fuata upepo, utafuata Kile unachokiamini na moyo wako
Nakumbuka Kuna watu wengi sana walichaguliwa masomo na kozi za Kusoma na Ndugu zao leo wanahangaika mtaani.Wamesubiri maghufuli afanye muujiza.
Usifanye kitu kumfurahisha Ndugu yako, fanya kwasababu Ndiyo maisha uliyoamua kuishi.
Imeandikwa na Adson Kagiye