Update:

25 August 2016

Ufaransa yapiga marafuku vazi la kiislamu ufukweni ‘burkini’

Mahakama kubwa nchini Ufaransa imeombwa kuiondoa marufuku iliyotolewa kwenye miji 26 nchini humo kuhusiana na wanawake wanaovaa nguo za kuogelea zinazofunika mwili mzima ufukweni. Vazi hilo linajulikana kama burkini.
AUSTRALIA-FRANCE-ISLAM-CLOTHING-MUSLIM-LIFESTYLE
Kundi la watetezi wa haki za binadamu limesema marufuku hayo ni kinyume na sheria za Ufaransa.
Mameya hasa kwenye fukwe za Riviera, wamesema marufuku hayo yanalinda utaratibu na sheria za umma.
Burkini-collage
Maoni mengi yanaonesha kuwa raia wa Ufaransa wamependa marufuku hayo lakini waislamu wanadai wanalengwa isivyofaa. Marufuku hayo yamewagawanyisha maofisa wa juu wa serikali ya Ufaransa.
Burkini ni nguo ya ufukweni inayoacha uso, mikono na miguu tu. Zimepigwa marufuku ili kuwa na utengano muhimu kati ya serikali na mambo ya kidini.
Maana yake ni kuwa watu wa dini na imani wako sawa chini ya sheria.